Moja ya maamuzi muhimu wakati wa ujenzi ni aina ya mabomba ya maji. Makosa hapa yanaweza kusababisha uvujaji, gharama kubwa za matengenezo, na hata uharibifu wa muundo wa nyumba.
PPR PIPE (Polypropylene Random): Bora kwa maji ya moto na baridi ndani ya nyumba. Haina kutu, muunganiko wake ni wa kudumu sana. Inastahimili shinikizo la juu.
GI PIPE (Galvanized Iron): Nzuri kwa mabomba ya nje na nguvu kubwa. Huanza kutu baada ya miaka 15-20 hasa maeneo ya pwani.
CHAGUA HIVI:
– Ndani ya nyumba (hot & cold water): PPR pipe
– Nje ya nyumba (main supply): GI pipe au HDPE pipe
– Maji ya jua (solar heater): PPR pipe lazima
– Maeneo ya pwani (Mapinga/Amani): PPR pipe ni bora
ANGALIZO: Angalia alama ya PN20 kwenye PPR pipe kwa maji ya moto. Nunua kutoka duka unalolimini.